Allah Mtukufu anasema kuhusu umuhimu wa kumtukuza Mtume (saww): ﴿ قُلْ بِفَضْلِ اللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا ﴾ “Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na kwa rehema Yake; basi kwa hayo waumini na wafurahie.” (Yunus: 58) Waumini walifurahia siku hiyo kwa dhikri, qaswida, mawaidha na kusoma historia ya Mtume (saww), kwa kutambua kwamba yeye ni neema iliyo kubwa kwa walimwengu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Sherehe kubwa na yenye baraka ya Maulid ya Mtume Muhammad (saww) iimefana mjini Nakuru, nchini Kenya. Sherehe hiyo ilihudhuriwa na waumini kutoka maeneo mbalimbali ya Kenya na Tanzania. Waumini hao walijumuika kwa ajili ya kuadhimisha tukio adhimu la Mazazi ya Mtume Muhammad Mustafa (saww), na kusikiliza mafundisho, elimu na maarifa yanayotokana na nuru yake tukufu (Rehma na Amani view juu yake na Kizazi chake kitoharifu).
Allah Mtukufu anasema kuhusu umuhimu wa kumtukuza Mtume (saww):
﴿ قُلْ بِفَضْلِ اللَّهِ وَبِرَحْمَتِهِ فَبِذَٰلِكَ فَلْيَفْرَحُوا ﴾
“Sema: Kwa fadhila ya Mwenyezi Mungu na kwa rehema Yake; basi kwa hayo waumini na wafurahie.” (Yunus: 58)
Waumini walifurahia siku hiyo kwa dhikri, qaswida, mawaidha na kusoma historia ya Mtume (saww), kwa kutambua kwamba yeye ni neema iliyo kubwa kwa walimwengu. Qur’ani inathibitisha:
﴿ وَمَا أَرْسَلْنَاكَ إِلَّا رَحْمَةً لِّلْعَالَمِينَ ﴾
“Na hatukukutuma isipokuwa uwe rehema kwa walimwengu.” (Al-Anbiyaa: 107)
Sherehe hizo pia ziliambatana na tukio jingine lenye baraka kubwa – Ndoa ya ndugu Hussein, kijana Mwislamu mpenda Mtume Muhammad (saww) na Ahlul Bayt wake (a.s). Hafla ya ndoa ilifanyika hapo hapo Nakuru, ikiunganishwa katika mazingira ya ibada, elimu na furaha ya Maulid.

Mtume Muhammad (saww) amesema kuhusu ubora wa ndoa:
- “Anayeoa amekamilisha nusu ya dini yake…”
- “Hakuna msingi uliowekwa katika Uislamu ulio pendwa zaidi kwa Allah kuliko Ndoa.”
Na katika Qur’ani:
﴿ وَمِنْ آيَاتِهِ أَنْ خَلَقَ لَكُم مِّنْ أَنفُسِكُمْ أَزْوَاجًا لِّتَسْكُنُوا إِلَيْهَا وَجَعَلَ بَيْنَكُم مَّوَدَّةً وَرَحْمَةً ﴾
“Na miongoni mwa ishara Zake ni kuwa Amekuumbieni wake kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao, naye ameweka baina yenu mapenzi na rehema.” (Ar-Rum: 21)
Kwa niaba ya waumini waliokuwepo, tunampongeza ndugu Hussein kwa kukamilisha mwongozo huu mtukufu wa Sunna ya Ndoa, hasa katika siku iliyojaa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwanga wa Umma, Mtume Muhammad (saww).
Sherehe hizi mbili—Maulid na Ndoa—zimeacha athari ya furaha, umoja na kuhuisha mapenzi kwa Mtume wa Rehma na Ahlul Bayt wake (a.s), na zimeimarisha hamasa ya waumini kuendeleza mafundisho yake katika jamii.

Your Comment